Bad Advertisement?

News / Reviews:
 • World News
 • Movie Reviews
 • Book Search

  Are you a Christian?

  Online Store:
 • Visit Our eBay Store • SWAHILI BIBLIA - LUKE 24

  JANA SURA - IJAYO SURA - AMARA


  24:1 Jumapili, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini wakichukua yale manukato waliyotayarisha.

  24:2 Walikuta lile jiwe limeviringishwa mbali na kaburi.

  24:3 Walipoingia ndani, hawakuona mwili wa Bwana Yesu.

  24:4 Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hilo, mara watu wawili waliovaa mavazi yenye kung`aa sana, wakasimama karibu nao.

  24:5 Hao wanawake wakaingiwa na hofu, wakainama chini. Ndipo wale watu wakawaambia, "Kwa nini mnamtafuta aliye hai kati ya wafu?

  24:6 Hayuko hapa; amefufuka. Kumbukeni aliyowaambieni alipokuwa kule Galilaya:

  24:7 `Ni lazima Mwana wa Mtu atolewe kwa watu waovu, nao watamsulubisha, na siku ya tatu atafufuka."`

  24:8 Hapo wanawake wakayakumbuka maneno yake,

  24:9 wakarudi kutoka kaburini, wakawapa mitume wale kumi na mmoja na wengine habari za mambo hayo yote.

  24:10 Hao waliotoa habari hizo kwa mitume ni: Maria Magdalene, Yoana na Maria mama wa Yakobo, pamoja na wanawake wengine walioandamana nao.

  24:11 Mitume waliyachukua maneno hayo kama yasiyo na msingi, hivyo hawakuamini.

  24:12 Lakini Petro alitoka, akaenda mbio hadi kaburini. Alipoinama kuchungulia ndani, akaiona tu ile sanda. Akarudi nyumbani huku akiwa anashangaa juu ya hayo yaliyotokea.

  24:13 Siku hiyohiyo, wawili kati ya wafuasi wake Yesu wakawa wanakwenda katika kijiji kimoja kiitwacho Emau, umbali wa kilomita kumi na moja kutoka Yerusalemu.

  24:14 Wakawa wanazungumza juu ya hayo yote yaliyotukia.

  24:15 Walipokuwa wakizungumza na kujadiliana, Yesu mwenyewe akatokea, akatembea pamoja nao.

  24:16 Walimwona kwa macho, lakini hawakumtambua.

  24:17 Akawauliza, "Mnazungumza nini huku mnatembea?" Nao wakasimama kimya, nyuso zao wamezikunja kwa huzuni.

  24:18 Mmoja, aitwaye Kleopa, akamjibu, "Je, wewe ni mgeni peke yako Yerusalemu ambaye hujui yaliyotukia huko siku hizi?"

  24:19 Naye akawajibu, "Mambo gani?" Wao wakamjibu, "Mambo yaliyompata Yesu wa Nazareti. Yeye alikuwa nabii mwenye uwezo wa kutenda na kufundisha mbele ya Mungu na mbele ya watu wote.

  24:20 Makuhani na watawala wetu walimtoa ahukumiwe kufa, wakamsulubisha.

  24:21 Lakini sisi tulitumaini kwamba yeye ndiye angeikomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu mambo hayo yalipotendeka.

  24:22 Tena, wanawake wengine wa kwetu wametushtua. Walikwenda kaburini mapema asubuhi,

  24:23 wasiukute mwili wake. Wakarudi wakasema kwamba walitokewa na malaika waliowaambia kwamba alikuwa hai.

  24:24 Wengine wetu walikwenda kaburini wakashuhudia yale waliyosema hao wanawake; ila yeye hawakumwona."

  24:25 Kisha Yesu akawaambia, "Mbona mu wapumbavu kiasi hicho na mioyo yenu ni mizito hivyo kusadiki yote yaliyonenwa na manabii?

  24:26 Je, haikumpasa Kristo kuteswa, na hivyo aingie katika utukufu wake?"

  24:27 Akawafafanulia mambo yote yaliyomhusu yeye katika Maandiko Matakatifu kuanzia Mose hadi manabii wote.

  24:28 Walipokikaribia kile kijiji walikokuwa wanakwenda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea na safari;

  24:29 lakini wao wakamsihi wakisema, "Kaa pamoja nasi, maana kunakuchwa, na usiku unakaribia." Basi, akaingia kijijini, akakaa pamoja nao.

  24:30 Alipoketi kula chakula pamoja nao, akachukua mkate, akaubariki, akaumega, akawapa.

  24:31 Mara macho yao yakafumbuliwa, wakamtambua; lakini yeye akatoweka kati yao.

  24:32 Basi, wakaambiana, "Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?"

  24:33 Wakaondoka saa ileile, wakarudi Yerusalemu: wakawakuta wale mitume kumi na mmoja na wale wengine waliokuwa pamoja nao, wamekusanyika

  24:34 wakisema, "Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simoni."

  24:35 Basi, hao wafuasi wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika kumega mkate.

  24:36 Wanafunzi wote wawili walipokuwa wakiwaambia hayo, Yesu mwenyewe akasimama kati yao, akawaambia "Amani kwenu."

  24:37 Wakashtuka na kushikwa na hofu wakidhani wameona mzimu.

  24:38 Lakini yeye akawaambia, "Kwa nini mnafadhaika? Mbona mnakuwa na mashaka mioyoni mwenu?

  24:39 Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo."

  24:40 Baada ya kusema hayo, akawaonyesha mikono na miguu.

  24:41 Wakiwa bado katika hali ya kutosadiki kwa sababu ya furaha yao, na wakiwa wanastaajabu, akawauliza, "Mnacho chakula chochote hapa?"

  24:42 Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa.

  24:43 Akakichukua, akala, wote wakimwona.

  24:44 Halafu akawaambia, "Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika Sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi."

  24:45 Kisha, akaziangazia akili zao ili wapate kuelewa Maandiko Matakatifu.

  24:46 Akawaambia, "Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na siku ya tatu atafufuka kutoka wafu,

  24:47 na kwamba ni lazima, kwa jina lake, mataifa yote kuanzia na Yerusalemu yahubiriwe juu ya kutubu na kusamehewa dhambi.

  24:48 Ninyi ni mashahidi wa mambo hayo.

  24:49 Nami mwenyewe nitawapelekeeni yule ambaye Baba aliahidi kumtuma, lakini ngojeni huku mjini mpaka mtakapopewa ile nguvu itokayo juu."

  24:50 Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki.

  24:51 Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni.

  24:52 Wao wakamwabudu, wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa:

  24:53 wakakaa muda wote Hekaluni wakimsifu Mungu.

  IJAYO SURA - BIBLIA MWELEZO & UTAFUTAJI

  God Rules.NET
  Search 100+ volumes of books at one time. Swahili Biblia Search Engine. Hausa Biblia Search Engine. Afrikaan Bible Search Engine